Atwoli achaguliwa tena naibu rais wa muungano wa vyama kimataifa

Taifa Leo - - News - Na Agewa Magut

KIONGOZI wa wafanyakazi nchini Francis Atwoli amechaguliwa tena kama naibu rais wa Muungano wa Kimataifa wa Vyama vya Wafanyakazi (ITUC) nchini Denmark.

Bw Atwoli, ambaye ni Katibu Mkuu wa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi Kenya (COTU), alichaguliwa tena jana wakati wa kongamano la nne la ITUC linaloendelea mjini Copenhagen.

Jina la mtetezi huyo wa haki za wafanyakazi nchini lilipendekezwa katika kongamano hilo la wajumbe zaidi ya 3,000, na viongozi wenzake kutoka mataifa ya Uganda, Rwanda, Burundi na Somalia.

Vile vile, alichaguliwa kama mwanachama wa Baraza Kuu la ITUC kuwakilisha kanda ya Afrika Mashariki.

Wajumbe waliunga mkono pendekezo la jina lake kwa pamoja, na kumtunuku kipindi kingine cha miaka minne katika uongozi wa ITUC, shirikisho ambalo anahudumu kama naibu rais kwa awamu ya tatu mfululizo.

“Wadhifa ambao mmenipa sio rahisi. Mnanituma vitani, kupigania haki za wafanyakazi kote ulimwenguni,” Bw Atwoli alisema.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Kenya

© PressReader. All rights reserved.