TSC yachunguza mwalimu kwa ubakaji

Taifa Leo - - News - Na GASTONE VALUSI

TUME ya Kuajiri Walimu Nchini (TSC) inachunguza naibu mmoja wa mwalimu mkuu wa shule ya msingi katika kaunti ndogo ya Yatta anayekabiliwa na tuhuma za kumbaka mwanafunzi wa Darasa la Nne.

Kisa hicho kiliibua kero kubwa katika eneo hilo huku raia wakitaka mwalimu huyo aadhibiwe vikali.

Mkurugenzi wa TSC kaunti ya Machakoa David Mukui jana alisema mshukiwa, Bw David Ngumbau, 49, alidaiwa kumbaka msichana huyo mwenye umri wa miaka tisa katika Shule ya Msingi ya Kyasioni mnamo Agosti 2, mwaka huu.

Alisema ingawa kesi hiyo iliripotiwa kwa TSC kuchelewa, tume hiyo imeanzisha uchunguzi.

“Tumeanza kuchunguzi tukio hilo na ikiwa itabainika kuwa mwalimu huyo alitenda uhalifu huo, hatua za kinidhamu zitachuliwa dhidi yake,” Bw Mukui akaongeza.

Mkurugenzi huyo wa TSC alisema mshukiwa alikamatwa Alhamisi na akafunguliwa mashtaka katika mahakama ya Kithimani mnamo Ijumaa.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Kenya

© PressReader. All rights reserved.