Kenya sasa yashauriwa kutumia teknolojia katika uzoaji taka mijini

Taifa Leo - - News - Na Collins Omulo

KENYA imetakiwa kuanza kutumia teknolojia katika uzoaji wake wa taka ili kupunguza ongezeko la taka katika miji mingi nchini.

Mkurugenzi wa Shirika la Usimamizi wa Majiji ya Afrika C40 Bw Hastings Chikoko – mtandao wa majiji makuu duniani yanayokumbana na changamoto za uzoaji taka – amesema kuwa majiji mengi Afrika hushindwa kuzoa taka kwa kuwa hakuna mbinu mwafaka kuhakikisha kuwa taka zinazotoka katika mitaa zime ka majaani.

Aliishauri serikali ya kaunti ya Nairobi kufuata mfano wa jiji la Addis Ababa, Ethiopia ambalo ndilo la kwanza Afrika kuwekeza katika kiwanda cha teknolojia au jiji la Durban, Afrika Kusini ambalo limefaulu kugeuza jaa lake kuwa la kisasa lenye eneo la burudani.

“Tunafaa kuta ti kuhusu teknolojia ambazo zinatumiwa na kuelewa jinsi ya kuboresha mbinu zetu za kuzoa taka huku tukitilia maanani mabadiliko ya tabianchi kwa kuwa taka huchangia gesi hatari katika mazingira yetu,” akasema Bw Chikoko.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Kenya

© PressReader. All rights reserved.