Bodi yakimbia kortini kujikinga dhidi ya vitisho vya kutimuliwa

Taifa Leo - - Habari Za Kaunti - Na David Muchui

BODI ya uajiri katika kaunti ya Meru imepata amri ya korti ya kuzuia bunge la kaunti hiyo kutimua wanachama wake, baada ya vitisho kutoka kwa madiwani.

Mnamo Jumatano, kamati ya Leba bungeni iliwasilisha ripoti ikilaumu bodi hiyo kuwa imekuwa ikiajiri watu kwa njia isiyofaa na kukosa kutii miito ya kufika mbele ya kamati za bunge.

Madiwani wenye ghadhabu walitaka bodi hiyo ivunjwe, wakidai kuwa ilitekeleza uajiri wa zaidi ya wafanyakazi 100 kwa njia isiyofaa. Lakini kupitia wakili Ken Muriuki, bodi hiyo sasa imetafuta kinga mahakamani katika kesi ambapo karani, spika na bunge la kaunti wameorodheshwa kama washtakiwa.

Bodi hiyo inataka bunge la kaunti kuzuiwa kutekeleza, kujadili ama kupitisha mswada wa kuwatimua wanachama wake hadi kesi isikizwe na kuamuliwa.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Kenya

© PressReader. All rights reserved.