Mbunge alalamikia uhaba wa walimu maeneo ya mashinani

Taifa Leo - - Habari Za Kaunti - Na Oscar Kakai

MBUNGE wa Kapenguria

Samuel Moroto ametoa wito kwa serikali kuajiri walimu wengi na kuimarisha elimu katika maeneo ya mashinani katika kaunti hiyo.

Bw Moroto alisema kuwa watoto wengi katika kaunti hiyo wako na kiu ya elimu lakini kuna shida ya uhaba wa walimu suala ambalo linachagia kiwango cha elimu kurudi chini.

Alisema kuwa eneo hilo lilitengwa kwa kipindi kirefu na kubaki nyuma kwa elimu kutokana na visa vya wizi wa mifugo,ndoa za mapema na ukeketaji.

“Tunaomba tume ya kuajiri walimu nchini TSC kuajiri walimu wa kutosha katika maeneo ya mashinani ili kuinua viwango vya elimu. Sisi kama viongozi hatuwezi kukaa kitako huku shule za eneo hili zikikosa walimu wa kutosha ili hali tume hiyo huajiri walimu kila mwaka,” alisema Bw Moroto.

Alisema kuna haja ya kujali maeneo yaliyotengwa na kuyapa kupau mbele kwa kuajiri walimu hasa kaunti ya Pokot Magharibi ambayo inaendelea kufanya vyema kwenye matokeo ya mitihani ya kitaifa.

Picha/maktaba

Mbunge wa Kapenguria Samuel Moroto.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Kenya

© PressReader. All rights reserved.