Nukuu za Wiki

Taifa Leo - - Kinaya -

“Cha muhimu zaidi ni kwamba nataka kusisitiza kuhusu ‘sera ya kurejea’, itakayowaelekeza walimu wakuu kuwapokea, kuwahifadhi na kuwasaidia wanafunzi wanaorejea shuleni. Tunahitaji kutafuta mbinu za kushughulikia visa hivyo (vya ujauzito wa wanafunzi) na kuwahakikishia watoto wote elimu,” Waziri wa Elimu, Bi Amina Mohamed, akisisitiza wanafunzi wanaojifungua wanapaswa kuruhusiwa kuendelea na masomo yao.

“Katika ripoti yake, kamati ya nidhamu ilipendekeza wabunge Aisha Jumwa (Malindi) na Suleiman Dori (Msambweni) wafukjuzwe chamani kwa utovu wa nidhamu. Baraza la kitaifa la chama (cha ODM) litawaita wanachama hao waliopendekezwa kufukuzwa wafike mbele yake katika kikao maalumu mwaka ujao kabla ya uamuzi wa mwisho kufanywa,” Katibu Mkuu wa ODM, Bw Edwin Sifuna.

“Nina ujasiri wa kubisha mlango huo (wa Ikulu) mara kadhaa, tena kwa sauti kuu, na siku moja mbingu itasikia na kujibu maombi yangu,” kiongozi wa chama cha Wiper, Kalonzo Musyoka, akieleza kuhusu ndoito yake ya kuwa rais wa Kenya siku moja.

“Wanaodhani siwezi kushirikiana na (Musalia) Mudavadi watashangaa sana. Nimejitolea kushirikiana naye ili kuhakikisha nguvu za wingi wa kura katika magharibi mwa nchi zinaleta manufaa,” Seneta wa Bungoma na kiongozi wa chama cha Ford – Kenya, Bw Moses Wetang’ula.

Zimekusanywa na DOUGLAS MUTUA

Newspapers in Swahili

Newspapers from Kenya

© PressReader. All rights reserved.