Elimu itiliwe mkazo Pwani

Taifa Leo - - Barua - MBOGOH SAMUEL MWAMBOGOH, Chuo Kikuu cha Maseno

ILI kufanikisha maendeleo Pwani, elimu ni kigezo cha kukumbatiwa na kuenziwa.

Ahadi aliyoitoa Gavana wa Kwale Salimu Mvurya ya kuwafadhili wanafunzi wote waliofuzu kujiunga na shule za upili za kitaifa ni jambo la kuigwa na magavana wote wa Pwani.

Inafaa viongozi wote eneo hili kushirikiana ili kulikomboa eneo hili ambalo husemekana jamii iko nyuma kielimu.

Ni vyema viongozi mbalimbali eneo la Pwani wajitokeze kuwafaa wanafunzi wote waliofanya vyema.

Kuwasaidia hawa watoto ni kuijenga Pwani ya siku za usoni.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Kenya

© PressReader. All rights reserved.