Mitandao yenye filamu za ngono inafaa izimwe kwa azma ya kuokoa watoto wetu

Taifa Leo - - Barua - EDWIN KARIUKI, Mombasa

NAUNGA mkono wazo kwamba Mamlaka ya Mawasiliano nchini idhibiti matumizi ya mitandao ili kuzima mitandao inayosambaza filamu za ngono. Mitandao hii imechangia watoto kushiriki ngono za mapema na kuwageuza wazazi wakiwa bado wachanga au wakati mwingine kuchangia wasichana kuavya mimba. Serikali yafaa kufunga mitandao hii ili kusaidia kizazi cha kesho. Utovu wa nidhamu umedhihirika miongoni mwa vijana wetu kutokana na video za ngono. Hata hivyo, ni jukumu la wazazi kuhakikisha wanajua ni nini watoto wao wanatafuta na kutazama kwenye simu zao. Isitoshe, wanafaa kudhibiti muda ambao watoto wao hutumia mitandaoni ili kuwapa maadili mema. Elimu ya uzazi vile vile inafaa kujumuishwa kwenye silabasi ili kuzuia janga hili.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Kenya

© PressReader. All rights reserved.