Kampeni za mapema zikome!

Taifa Leo - - Barua - SAMMY KAMANDE, Kenya Coast National Polytechnic

VIONGOZI wanaolenga kuwania vyeo mbalimbali nchini wameanza kupiga debe kuhusu siasa za mwaka 2022 badala ya kukamilisha ajenda walizoahidi wananchi uchaguzini 2017.

Hatua hii inazorotesha maendeleo kwa kuwa wanatumia pesa nyingi za umma kujiombea kura kwa sasa, ambazo zingefaa katika kuboresha miundomsingi.

Viongozi hawa hususan walio madarakani wanafaa kutekeleza waliyoahidi wananchi kwenye uchaguzi uliopita, kwani hii ndiyo njia bora pekee ya kurudishwa madarakani na mwananchi.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Kenya

© PressReader. All rights reserved.