Ujumbe Mfupi

Taifa Leo - - Barua -

MAONI: WAZEE wa jamii ya Kalenjin wamelalamika kwamba juhudi za kumpatanisha Naibu Rais William Ruto na Seneta wa Baringo Gideon Moi zimefeli, kwa sababu wawiki hao wanajiona ni “wakubwa sana” na hawaachi vita vyao vya ubabe kuhusu uongozi wa Rift Valley. Je, kuna haja ya kupatanisha viongozi hao wawili iwapo wamekuwa vichwa ngumu?

Hamna haja kupatanisha mahasidi hawa wa kisiasa kwa sababu wote wana lengo moja: kuwa wenyeji wa ikulu. Wakati Ruto anajitetea kutoka kabila la umasikini naye Moi anajigamba kama mwana Kanu, chama kilichowalea wote kisiasa na chenye kushutumiwa kwa uongozi uliojaa dhuluma nchini. Kwa sababu wote wanataka kuonyesha ubabe wa kisiasa, tamaa ya kuingia ikulu na usemi katika jamii ya Kalenjini juhudi zozote za kuwaleta pamoja zitakua sawa na kupigia mbuzi gita. Aidha wazee hao wamesahau walivyonena malenga, vita vya panzi furaha kwa kunguru. Jonah Rwigi, Kiritiri

Kama wameshindwa kupatana waachwe vivyo hivyo kwani wao ni watu wazima na wanajipigania wao wenyewe. Ni kila mmoja na msalaba wake. Charo Mzee kutoka Embu Hakuna haja ya patanisho kwani mpiga kura ndiye atakayeamua ni yupi bora atakayetetea maslahi na kutimiza matakwa yake mwananchi mlalahoi. Jim Iladiva

Hakuna haja. Wazee wanaweza kupatanisha madiwani ama wabunge lakini si hawa watu wawili wanaolenga viti vikubwa. Joze Mukubio Limiri

Ipo haja ya kuwapatanisha viongozi hao kwa sababu ndiyo njia pekee ya kuleta amani kati yao na vile vile wafuasi wao. Brian O'neal, kupitia fbook

Wakenya hawako tayari kuchagua mmoja kuwa rais wa Kenya. kwa hivyo waachwe waendelee kupambana, hakuna haja ya kuwapatanisha. Ndunda Joseph MJADALA WA LEO: NAIBU Rais William Ruto na baadhi ya viongozi kutoka Rift Valley wamekashifu mamlaka za kupambana na ufisadi, wakisema zinaegemea maeneo fulani katika vita hivyo na kuingiza siasa. Je, kuna ukweli wowote katika tetesi zao ama wanaogopa kwamba vibaraka wao wamenaswa na mtego wa wapelelezi?

Newspapers in Swahili

Newspapers from Kenya

© PressReader. All rights reserved.