Walofa mtaani wamfukuza demu wakidai anawazuzua na kuwapora

Taifa Leo - - Dondoo! - Na John Musyoki

VIJANA mtaani hapa walimtimua kipusa mgeni wakimlaumu kwa kuwanyemelea na kuwapora. Duru zinasema demu huyo ni mrembo ajabu na kila mwanaume alikuwa akimtamani hasa vijana wa mtaani.

Yadaiwa tangu alipokita kambi sehemu hii, vijana walianza kumiminika katika chumba chake.

Kabla ya siku ya kioja ripoti zilienea kuwa demu huyo alikuwa akiwapagawisha vijana na kuwapora.

Ilidaiwa kuwa licha ya kuwazazua vijana hakuna aliyebahatika kuonja asali huku wakishuku kwamba alikuwa akitumia ndumba. Baada ya vijana kulalamika kwa muda mrefu waliungana pamoja na kuamua kumtimua mwanadada huyo. Inasemekana walikita kambi plotini na kumwamuru arudi kwao.

"Kuanzia leo hautaishi hapa. Umekuwa ukituchezea akili sana na kutupora. Umetudaganya kwa muda mrefu," jamaa mmoja alisikika akisema.

"Demu huyo ni mshirikina. Nilimpatia pesa zangu lakini sikuonja asali hata kidogo. Tumtimue mbio hata hana maana," jamaa mwingine alisema.

Lakini demu alijitetea: "Mimi sio mtu wa kurukiwa hivi hivi. Kama mnataka niondoke ni sawa lakini mtanitafuta hivi karibuni na mtu akijaribu kunigusa au mali yangu atajuta," demu alisema.

Inasemekana demu alifunganya virago vyake na kuondoka huku majamaa wakipigwa na butwaa baada ya kuwaambia hivyo.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Kenya

© PressReader. All rights reserved.