Vipusa wamzima jombi aliyewakosoa kanisani

Taifa Leo - - Dondoo! - Na Richard Maosi

kioja katika kanisa moja mtaani hapa akina dada walipomkemea kalameni aliyewakosoa akitoa ushuhuda.

Ripoti zinasema jombi alibadilisha ibada na kuanza kuwasuta akina dada wa kanisa hilo akisema walikuwa wamevalia ngozi ya kondoo ilhali moyoni ni mbwa mwitu.

Duru zasema vipusa walimkatiza na kudai aliwasuta kwa kukataa kumeza chambo alipowarushia mistari ya mapenzi. “Vipusa hawakumruhusu kuendelea na ushuhuda aliposema alikuwa dume kamili na hakuwa amepungukiwa na vidosho wa kuchumbia,” alisema mdokezi. Mchungaji wa kanisa hilo aliwatuliza vipusa hao na kuwaambia hawakufaa kupiga kelele kanisani.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Kenya

© PressReader. All rights reserved.