Ishara za muungano mkubwa usiozuilika

Wadadisi wahisi ni rahisi kuvumisha muungano kati ya Moi, Mudavadi, Kalonzo sababu hawana kashfa na wanatoka maeneo ya idadi kubwa ya wapigakura

Taifa Leo - - Jamvi - Na BENSON MATHEKA

HUENDA muungano wa kisiasa ukaibuka kati ya mwenyekiti wa chama cha Kanu Gideon Moi, kiongozi wa chama cha Amani National Congress (ANC) Musalia Mudavadi, mwenzake wa Wiper Kalonzo Musyoka na hata kiongozi wa chama cha ODM Raila Odinga kabla ya uchaguzi mkuu wa 2022.

Wadadisi wanasema wanasiasa hao wamekuwa wakichangamkiana tangu muafaka kati ya Rais Uhuru Kenyatta na Bw Odinga mapema mwaka huu na matamshi ya wandani wao wa kisiasa yanaonyesha kuna uwezekano wa kuungana kisiasa.

Majuzi, wabunge wa eneo la Magharibi mwa Kenya walimuomba Bw Moi kuungana na Bw Mudavadi na Bw Musyoka kubuni muungano wa kisiasa ambao utaunda serikali baada ya uchaguzi mkuu wa 2022.

mstaafu Daniel Moi, baba yake Gedion.

“Hao ni kama watoto wa baba mmoja kisiasa. Walikuzwa kisiasa na Mzee Moi na wana tabia zinazofanana. Ni rahisi kwao kushirikiana kisiasa. Hata hivyo, tatizo ni kuwa huenda wakakosa ushawishi unaohitajika iwapo kutaibuka muungano mwingine thabiti,” alisema mchanganuzi wa siasa, Daisy Kamau.

“Nafikiri wanaelewa udhaifu wao na ndio sababu wanamikakati wao wanawashauri waungane na kiongozi wa chama cha ODM Raila Odinga au wapate baraka za Rais Kenyatta ili kuzima kabisa muungano unaoweza kubuniwa na Naibu Rais William Ruto,” aliongeza Bi Kamau.

Bw Moi, Bw Mudavadi na Bw Musyoka wametangaza azima yao ya kugombea urais kwenye uchaguzi mkuu wa 2022 na wadadisi wanasema ikiwa wataungana, mtihani utakuwa nani kati yao atapeperusha bendera yao.

“Lililo wazi ni kuwa huu muungano unapikwa, japo uchaguzi utakuwa miaka minne ijayo. Ndio sababu umekuwa ukimsikia Bw Moi akitaka wafuasi wa Bw Mudavadi na Bw Musyoka wamruhusu viongozi hao kushirikiana naye kufanya kazi,” aeleza Bw Charles Ouma, mdadisi wa siasa.

Akiwa eneo la Kakamega, Bw Moi aliwaomba wakazi wa eneo hilo kumruhusu ashirikiane na Mudavadi kisiasa sawa na alivyowaomba wakazi wa Kitui alipohudhuria mazishi ya babake Musyoka Musyoka mwezi uliopita.

Bw Moi ambaye anapigania ubabe wa kisiasa na Bw Ruto eneo la Rift Valley pia alitembelea eneo la Nyanza, ngome ya kisiasa ya Bw Odinga ambaye hajatangaza wazi iwapo atagombea urais 2022.

Hata hivyo, washirika wa Bw Odinga wakiongozwa na seneta wa Siaya James Orengo waliandamana na Bw Moi katika hafla moja Kaunti ya Kakamega wiki jana ambapo alitakiwa kushirikiana na Bw Mudavadi na Bw Musyoka kuendeleza azma zao za kisiasa.

Ishara kwamba muungano kati ya ODM, KANU, ANC na Wiper unasukwa, ni mikutano ambayo Bw Moi amekuwa akifanya na Bw Odinga, Mudavadi na Kalonzo Musyoka. Pia mapema mwaka huu, alikutana na naibu kiongozi wa chama cha ODM Hassan Joho

Mbunge wa Lurambi Titus Khamala, seneta wa Kakamega Cleophas Malala, Seneta wa Baringo Gideon Moi, kinara wa ANC Musalia Mudavadi, Mbunge wa Saboti Caleb Amisi na viongozi wengine wakiwa katika shughuli ya kuchanga pesa mjini Kakamega wikendi iliyopita.picha/

na wakatangaza kuwa washirikiana kisiasa.

Viongozi hao wote pia wamekutana na Mzee Moi nyumbani kwake Kabarak. Kulingana na mbunge maalumu Godfrey Osotsi vyama vya ODM, ANC, Kanu na Wiper vinapanga mikakati ya kutafuta mrithi wa Rais Kenyatta.

“Tunaweka mikakati ya kuwaandaa wafuasi wetu kabla ya kuamua nani atakuwa nani. Vigogo wa kisiasa kutoka maeneo yote wataketi na kutupatia mgombea urais,” Bw Osotsi alisema.

Bw Ouma anasema muungano wa viongozi hao unaweza kukubalika nchini wakijivumisha kwa wapiga kura kama wanasiasa wasio na doa.

“Kufikia sasa, hawajahusishwa na sakata yoyote inayoweza kuwapaka matope tofauti na baadhi ya wanasiasa wengine wanaoweza kuwa wanamezea mate urais. Unaweza kuwa muungano thabiti kwa kutegemea makubaliano na malengo yao,” aeleza Bw Ouma.

Hata hivyo, anasema siasa za Kenya ni telezi sana na chochote kinaweza kutokea kabla ya 2022.

Bw Mudavadi amenukuliwa akisema kuwa atashirikiana na wanasiasa wanaotaka kuimarisha maisha ya Wakenya akiwemo Bw Moi aliyemtaja kama rafiki wa siku nyingi.

“Tuna historia ndefu na sina shida kufanya kazi na Bw Moi. Hata hivyo, ninaomba wakazi Kinara wa Amani National Congress (ANC) Musalia Mudavadi na mwenzake wa Wiper Kalonzo Musyoka wakishauriana kwenye ha a ya awali.

wa ngome yake kuniunga mkono kwa sababu kwa miaka 24 eneo la Magharibi lilimuunga mzee Moi kwa uaminifu,” Bw Mudavadi alisema.

Wadadisi wanasema muungano wowote utakaohusisha Bw Moi utalenga kumzima Bw Ruto ambaye ndiye hasimu wake mkuu wa kisiasa eneo la Rift Valley ambalo lina kura nyingi.

“Muungano utakuwepo na utakuwa dhidi ya Bw Ruto ambaye pia amepenya ngome za upinzani na kuwashawishi wanasiasa kadhaa kumuunga mkono,” aeleza Bw Ouma

Anatoa mfano wa eneo la Magharibi ambapo Bw Ruto amefaulu kuwanasa wabunge kadhaa akiwemo aliyekuwa

seneta wa Kakamega Boni Khalwale anayedai kuwa mipango ya Mudavadi kuungana na Bw Moi itafanya eneo hilo kubaki katika upinzani 2022.

Bw Osotsi anahisi kwamba ni rahisi kuvumisha muungano kati ya Moi, Kalonzo na Mudavadi kwa sababu hawana kashfa zozote na wanatoka maeneo yaliyo na idadi kubwa ya wapigakura.

Kulingana na Bi Kamau, muungano kati ya Moi, Mudavadi, Musyoka bila baraka za Raila au Rais Kenyatta unaweza kukabiliwa na upinzani mkali.

Seneta wa Kaunti ya Baringo Gideon Moi na Kinara wa ANC Musalia Mudavadi (kulia) wakionyesha furaha kuu walipokutana wakati wa shughuli ya kuchangisha pesa za kununuliwa wafanyabiashara basi mjini Kakamega wikendi iliyopita. Picha/ Maktaba

Newspapers in Swahili

Newspapers from Kenya

© PressReader. All rights reserved.