12 wafariki kwenye makabiliano ya risasi kati ya polisi na wezi

Taifa Leo - - Habari Za Afrika Na Dunia -

WATU 12, wakiwemo mateka watano, waliuawa kaskazini mwa Brazil baada ya polisi kutibua njama ya majambazi kupora benki mbili katika mji wa Milagres, maafisa walisema.

Mateka hao watano walikuwa watu wa familia moja na walijumuisha watoto wawili, meya wa mji huo Lielson Landim aliambia gazeti la Folha de Sao Paulo Ijumaa.

Walikamatwa na baadhi ya majambazi hao waliokuwa wakirejea kutoka uwanja wa ndege ulioko karibu.

Waziri wa usalama katika jimbo la Ceara, Andre Costa, alisema kupitia taarifa kwamba uchunguzi unaendeshwa kwa lengo la kuwatambua waliouwa na kilichosababisha vifo vyao.

Costa hakubaini ikiwa watu hao sita waliuawa kwa risasi iliyofyatuliwa na majambazi au polisi. Awali, meya Landim alikuwa amesema kuwa kwa mujibu habari zilizopokelewa na afisi yake, “wahalifu waliwaua mateka na polisi wakawaua wahalifu hao.”

“Wanachama wa kundi moja lenye silaha liliwasili katika mji huo Ijumaa jioni na ndipo wanatekeleza uhalifu huo. Kulitokea ufyatulianaji wa risasi kati ya washukiwa na polisi, “taarifa hiyo ilisema.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Kenya

© PressReader. All rights reserved.