Mahakama yaidhinisha Rais kuwania kwa muhula wa tatu

Taifa Leo - - Habari Za Afrika Na Dunia -

RAIS wa Zambia Edgar Lungu, sasa anaweza kuwania urais kwa awamu ya tatu katika uchaguzi mkuu ujao wa mwaka wa 2021, Mahakama ya Kikatiba imeamua.

Rais wa mahakama hiyo Hilda Chibomba alisema uamuzi huo uliotolewa Ijumaa na majaji saba wa mahakama ulikuwa ni wa pamoja.

“Jibu letu ni kwamba muhula wa kwanza wa Rais Lungu hauwezi kuchukuliwa kuwa muhula kamili,” Chibomba akasema alipotangaza uamuzi huo.

Vyama vinne vya kisiasa vilikuwa vimewasilisha kesi katika mahakama hiyo vikitaka Rais Lungu azuiwe kuwani urais katika uchaguzi mkuu ujao vikisema hiyo itakuwa kinyume cha Katiba. Kulingana na Katiba ya Zambia mtu hawezi kushikilia urais kwa zaidi ya mihula miwili.

Rais Lungu alichaguliwa kwa mara ya kwanza mnamo Januari 2015 baada ya kifo cha Rais wa zamani Michael Sata. Alihudumu kwa mwaka moja na miezi sita katika muhula wake wa kwanza uongozini.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Kenya

© PressReader. All rights reserved.