Wanajeshi 9 wauawa na magaidi shambulioni

Taifa Leo - - Habari Za Afrika Na Dunia -

WANAJESHI tisa wa Somalia, wakiwemo majenerali wawili, waliuawa kwenye mlipuko uliotokea nje ya mji mkuu Mogadishu, wapiganaji wa kigaidi na maafisa wa jeshi la Somalia walisema.

Kundi la kigaidi la Al-shabaab lilidai kuhusika katika shambulio hilo lililotokea Ijumaa asubuhi. Kupitia taarifa, magaidi hao walisema kuwa walifaulu kuharibu gari moja aina ya pick-up ambalo lilikuwa likiwasifirisha wakuu wa jeshi na walinzi wao karibu na kijiji cha Dhanaane, viungani kwa Mogadishu.

Msemaji wa Al-shabaab Abdiasis Abu Musab aliwatambua wakuu wa jeshi waliouawa kama; Omar Aden na Adi Ali.

Afisa mmoja wa jeshi la Somali ambaye alijitambulisha kama Kapteni Mohamed alithibitisha kuwa majenerali wawili na walinzi wao waliuawa huku wengine wakijeruhiwa.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Kenya

© PressReader. All rights reserved.