Sita wafa klabuni kwa kukanyagwa na waliokuwa wakihepa

Taifa Leo - - Habari Za Afrika Na Dunia -

sita walifariki jana alfajiri katika mkanyagano uliotokea ndani ya klabu moja katika kitongoji cha Ancona kati mwa Italia, wazimamoto walisema.

Wengine wengi,hususan vijana, walijeruhiwa wakitoroka harufu mbaya iliyotokana na kuvuja kwa mojawapo wa mitungi ya gesi.

Duru zalisea kuwa takriban watu 1,000 walikuwa ndani ya klabu hiyo kwa jina Blue Lantern iliyoko katika mji wa Corinaldo. Walikuwa wakitumbuizwa na mwanamuziki wa mtindo wa rappa Sfera Ebbasta.

“Tulikuwa tukisakata densi tukisubiri shoo yenyewe kuanza ndipo tukavamiwa na harufu kali ya gesi hatari,’ mvulana mwenye umri wa miaka 16 ambaye alikimbizwa hospitalini baada ya kuzirai, aliwaambia wanahabari.

“Tulikimbilia katika mojawapo ya milango lakini ilikuwa imefungwa. Walinzi walituambia turudi ndani na ndipo baadhi yetu tukaanguka na kukanyagwa,” akaongeza.

Picha/ AFP

WAOKOAJI nchini Italia wakiwapa huduma ya kwanza baadhi ya walionusurika katika mkanyagano ndani ya klabu jana.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Kenya

© PressReader. All rights reserved.