Nyota

Taifa Leo - - Fumbo & Falaki - Na Sheikh Khabib

KONDOO Machi 21 – Aprili 20: Ni siku chache tu zimebaki milango yako ifunguke, heri iko njiani. Huu ndio wakati mzuri wa kushughulikia safari au kazi iliyokwama kwa sababu bahati iko upande wako. Fanya hivyo mara moja.

NG’OMBE Aprili 21 – Mei 20: Hii ni siku ya bahati kubwa sana kwako. Utashangaa sana kwani watu wengi watakuchangamkia na watakuwa radhi kukufaa na kusuluhisha matatizo yako. Kuna milango itafunguka lakini kumbuka hujui bahati itadumu hadi lini.

MAPACHA Mei 21 – Juni 21: Umekataa kuwaadhibu waliokukosea kwa muda, na huenda ukajuta kwa hatua hiyo. Pia una nafasi nzuri ya kutimiza jambo la kimapenzi lakini unachelea kuchukua hatua kwa kuogopa fedheha. Itabidi upige moyo konde iwapo unataka kufaulu.

KAA Juni 22 – Julai 22: Nyota yako yasema unahitaji ushauri wa wataalamu kwa dharura. Kutimia kwa mipango uliyonayo wakati huu kunategemea jinsi utahusisha watu wengine kwani wewe pekee hujiwezi. Hata hivyo, jitenge na malofa.

SIMBA

Julai 23 – Agosti 22:

Imekuwa vigumu kwako kuamua jambo fulani. Umejipata katika njia panda inayokutenganisha na utajiri na umaskini na ni juu yako ujue la kufanya ili kuhakikisha kuwa umechukua njia inayokuelekeza kwa utajiri. Zingatia utulivu.

MASHUKE

Agosti 23 – Septemba

23: Unakumbushwa kuwa maadui ni wengi, lakini kuwa na mtu wa moyo mkunjufu leo kutakufaa zaidi kwani unaweza kukutana na mtu mgeni na muwe marafiki kwa manufaa yako. Jieleze vya kutosha katika mazungumzo yenu. Usidanganye hata kidogo.

MIZANI

Septemba 24 – Oktoba

23:Bado kuna nuru. Nyota yako hii itakuletea mabadiliko mengi katika maisha yako hivi karibuni. Yakikufika yakubali tu, yawe ni mazuri au ni mabaya. Hatimaye utamakinika useme yaliyojiri yalikuwa na athari nzuri kwako.

NGE

Oktoba 24 – Novemba

22: Matatizo mengi unayoona yakikuandama yanatokana na nuksi ambayo imeingia nyumbani kwako. Tafuta namna ya kuondoa nuksi hiyo kabla haijaenea. Lakini ni lazima uweke kila jambo kwenye mizani ili uamuzi wako uwe sahihi zaidi.

MISHALE

Novemba 23 – Desemba

21:Umekuwa mhisani kwa kila mtu na kwa sababu hiyo kuna watu wanaokutafuta wakitaka msaada kutoka kwako kila mara. Lakini inaonekana hutaki kuwasaidia. Itabidi uwajulishe umebadili msimamo wako lau sivyo bahati uliyonayo itakuponyoka.

MBUZI

Desemba 22 – Januari 20:Umekuwa

ukitumia vibaya pesa zako katika siku za hivi majuzi hivi kwamba umeshindwa kutimiza baadhi ya mahitaji muhimu ya jamaa zako. Jaribu kujitenga na marafiki wabadhirifu iwapo unataka kufaulu maishani.

NDOO

Januari 21 – Februari

19: Leo jiepushe na marafiki wengi au maeneo yenye kelele kwani mawazo uliyonayo yanahitaji utulivu. Ikiwezekana barizi na umpendaye na huenda ukapata utatuzi wa shida yako.

SAMAKI

Februari 20 – Machi

20:Huu ni wakati mzuri wako kutafakari kuhusu maisha yako ya baadaye. Weka kando mambo yasiyo na maana kwa sasa kwani maisha yako ni muhimu zaidi ya jingine lolote duniani.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Kenya

© PressReader. All rights reserved.