Amenitelekeza ghafla

Taifa Leo - - Fumbo & Falaki -

Hujambo Shangazi. Nimekuwa na uhusiano na mwanamume fulani kwa miaka sita sasa na amekuwa akila pesa zangu tu. Sasa amenipa mimba na ananiambia hayuko tayari kuoa. Yeye anaishi Nairobi nami naishi Mombasa. Je, atanioa au la? Kupitia SMS

Hujaelezea ni kwa nini amekuwa akila pesa zako ilhali yeye ndiye mwanaume anayefaa kukupa pesa za kugharamia mahitaji yako. Pili, sielewi ilikuwaje ukakubali kupata mimba yake bila hakikisho kutoka kwake kwamba atakuoa. Madai yake kuwa hayuko ni dalili za kutaka kujitenga nawe na usishangae akikutema. Ushauri wangu ni kuwa uwe tayari kwa chochote kile kutoka kwake.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Kenya

© PressReader. All rights reserved.