Mpenzi hanitaki tena

Taifa Leo - - Fumbo & Falaki -

Shikamoo Shangazi. Nina umri wa miaka 20 na nimekuwa na mpenzi kwa miaka miwili sasa. Sasa amenigeuka ghafla ananiambia eti hanitaki nitafute mwingine. Nampenda sana na sijui nitafanya nini. Naomba ushauri wako. Kupitia SMS

Ni muhimu ufahamu kuwa hakuna mikataba inayowekwa kudumisha uhusiano kwa hivyo mmoja wa wahusika akihisi kujiondoa kwa sababu moja au nyingine ana haki ya kufanya hivyo. Kama mwenzako amekwambia hakutaki, huna la kufanya ila kukubali uamuzi wake kwa sabu huwezi kumlazimisha akupende.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Kenya

© PressReader. All rights reserved.