Ng’ombe hula nyasi

Taifa Leo - - Ushairi Wenu -

Twasimama wimawima, maghulamu kutangaza,

Tuandame himahima, mkione kiwajuza, Kiwatie hemahema, matokeo mwanze waza, Twajua munafahamu, ng`ombe hawa hula nyasi.

Haikuwa hivi zama, wa usoni yatumiza, Asubuhi na mapema, ng’ombe nyasi anajaza, Kesho yetu sio wima, nani atatuuguza, Twajua munafahamu, ng`ombe hawa hula nyasi. Amesaliya kuchuma, taa kizima mwangaza, Miji kisalia nyuma, na tumbo zao kujaza, Kiwapa yenu lawama, kunyamaa mwawagiza,

Twajua munafahamu, ng`ombe hawa hula nyasi.

Nne tunatia koma, maghulamu twanyamaza,

Uongozi ni gharama, ni msemo twawajuza, Tenda mema kijituma, machoni wondoe kiza,

Twajua munafahamu, ng’ombe hawa hula nyasi. PETER WANJOHI ‘Kitunguu Machoni’ Nairobi

Newspapers in Swahili

Newspapers from Kenya

© PressReader. All rights reserved.