Genge lao

Taifa Leo - - Ushairi Wenu -

Wako wapi mashujaa, maisha waloyadhuru, Taifa kupigania, kudai wao uhuru, Walozikana fadhaa, taifa likawa huru, Simba walipofariki, itazame ngao yao!

Walobaki hawawezi, hawawezi kuongoza, Badala yake ni wezi, taifa wameliuza, Waliaga wakombozi, uhuru tukapoteza, Simba walipofariki, itazame ngao yao!

Wengi wamewakatisha, wamepigwa marisasi, Wakapoteza maisha, twaona utusitusi, Wengine wamewatisha, wakisema ni risasi, Simba walipofariki, itazame ngao yao!

Bayana wanatutenda, usiku wote na mchana, Nazo bei zimepanda, huku wao wakivuna,

Uchumi umetushinda, haujawa jambo sena, Simba walipofariki, itazame ngao yao!

ATANG’A CLERKSON ‘Sumu Tamu’ Nairobi

Newspapers in Swahili

Newspapers from Kenya

© PressReader. All rights reserved.