Tupate wapi ajira?

Taifa Leo - - Ushairi Wenu -

Nauliza jamaneni, kwa nini ninajitoma, Nauliza nambieni, mbona mimi ninasoma, Nauliza nelezeni, nitakula nyama choma? Kuuliza si ujinga, tafadhali nelezeni.

Nauliza kwa upole, si mimi ni mlokole, Nauliza mbona yale, nipate ona miale, Nauliza mkatale, Bongopevu nisilale, Kuuliza sii ujinga, tapata wapi ajira?

Nauliza mara tena, kuhusu hizi ajira, Nauliza nini sina, nimekuja na shajara, Nauliza je vijana, tutaja kuwa vinara? Kuuliza si ujinga, tapata wapi ajira.

Nauliza hamwamini, tutaijenga uchumi,

Nauliza mwatuhini, hatutawapiga ngumi,

Nauliza hamuoni, tuna vyeti vya usomi,

Kuuliza si ujinga, tapata wapi ajira.

AGGREY BARASA ‘Bongopevu’ MMUST, Kakamega

Newspapers in Swahili

Newspapers from Kenya

© PressReader. All rights reserved.