Nani alaumiwe?

Taifa Leo - - Ushairi Wenu -

Umekolea usasa, dunia kaigeuza,

Usasa sililo kosa, ila maadili kuoza,

Makosa ya nani hasa? heshima kuomboleza, Maadili kuzorota, ni nani alaumiwe?

Tamaduni tuikuze, wahenga tuwathamini, Taadhima tuwajuze, kuanzia kiamboni, Wavyele tusisitize, adhabu tuwajuzeni, Maadili kuzorota, ni nani alaumiwe?

Tusiwatusi viongozi, kuwafanyia dhihaka, Pia wao ni wazazi, watutwalie baraka, Wazazi na viongozi, chuja mnayotamka, Maadili kuzorota,ni nani alaumiwe?

Kwaherini sina mengi, nilosema so utesi, Elimu ndio msingi, wa maisha yetu sisi, So busara ilo nyingi, viongozi kuwatusi, Maadili kuzorota, ni nani alaumiwe? MIKE SIMIYU Naivasha

Newspapers in Swahili

Newspapers from Kenya

© PressReader. All rights reserved.