Akili ni mali

Taifa Leo - - Ushairi Wenu -

Pindi ukitawakali, hoja na huja kutowa, Kaachi utaamali, siboronge kubomowa, Kalima si dhalalali, semo semi kitongowa, Kisemi semo menowa, kwamba akili si mali.

Zalizo zama azali, wajuvi na wasojuwa, Nyeti semo medalali, mazinduzi kuzinduwa, Kisemo hino methali, kwamba akili ni mali, Ukwasi metajiriwa, za nasaha mbalimbali.

Wingi zililo galili, kadiri kukadiriwa,

Bongo wazo kusaili, fanifa mafanikiwa, Zama fanifa akili, sarafu mesarifiwa, Ndizo zinazogutiwa, kwamba akili ni mali.

Hichi ni kisemi ghali, adimu kukinunuwa,

Na wapo hukikubali, wabeza kukibeuwa, Kimekuzinga zohali, huishi kukifafanuwa, Humudu kun'gamuwa, kisemo akili ni mali. ABDALLA SHAMTE DP ‘Mtumwa wa Mungu’ Mwembekuku, Mombasa

Newspapers in Swahili

Newspapers from Kenya

© PressReader. All rights reserved.