Kiwa kweli wampenda

Taifa Leo - - Ushairi Wenu -

Hebu wake niweleze, yale ya kuzingatia, Yafaa mtekeleze, ndoa ifuate njia,

Mume kwanza umuwaze, kazini akiishia, Haya kiyatekeleza, moyoni atakuweka.

Moyoni atakuweka, chakula kimpikia, Mavazi yakichafuka, upesi kamfulia,

Isiwe lako kufoka, nyumbani akiingia, Mpokee kwa upendo, naye kwako ataganda.

Naye kwako ataganda, siri zenu kihifadhi, Simfanye akakonda, wala ukampa maradhi, Tusimwone amerunda, kwa unayomkabidhi, Na mara anyamazapo, mwulize linomsibu.

Mwulize linomsibu, ukiwa mnyenyekevu, Kumcheka sijaribu, kuwa tu mwenye utuvu, Kumkanda ujaribu, ili apate utulivu,

Yapo ya kumfanyia, ‘kiwa kweli wampenda. DENNIS SHONKO ‘Sonko’ Naivasha

Newspapers in Swahili

Newspapers from Kenya

© PressReader. All rights reserved.