Msiba ulotusibu

Taifa Leo - - Ushairi Wenu -

Rabuka ulo Manani, Muumba ulo kamili, Nakuomba Mkawini, ipunguze hii hali, Tuondoshee huzuni, japo tumeshakubali, Imetuwia muhali, majonzi kuyakabili. Pumzika kwa amani, somo yangu Matishali, Kwani mwako maishani, uliyafanya aali, Na sote tukabaini, utu sio kitu ghali,

Ilo thabiti kauli, nakwombea kwa Manani.

Machozi tele machoni, nalia Shaban Ali, Na huzuni kifuani, tena nyingi si kalili, Nakuomba Mkawini, huko kufanye sahali, Kwa mkono wa Shemali, kitabuche usimpe.

Hukukiweka moyoni, kinyongo Mzee Ali,

Sote tulikuthamini, kwa kuupenda ukweli, Zinanifaa yakini, zile za kwako kauli,

Tena zina kubwa dhima, najivuna sana babu.

Kwendelea natamani, moyo haujakubali, Chozi ladondoka chini, tungo naiweka mbali, Tatu ongeza thineni, hapo natia kufuli, Ningalipewa asali, la furaha silioni. MOHAMMED SHABAN ALI ‘Mpembuzi’ Mkomani

Newspapers in Swahili

Newspapers from Kenya

© PressReader. All rights reserved.