Ishara zaonyesha Pochettino ndiye chaguo la Manutd

Taifa Leo - - Spoti -

KOCHA Mauricio Pochettino, 46, anaongoza orodha ya wakufunzi wanaopigiwa upatu kuirithi nafasi ya Jose Mourinho uwanjani Old Trafford msimu ujao iwapo kikosi hicho kitashindwa kufuzu kwa kipute cha UEFA msimu ujao.

Hata hivyo, mkufunzi huyo mzawa wa Argentina amesisitiza kwamba hana nia ya kubanduka kambini mwa Tottenham Hotspur ambao kwa sasa wanamdumisha kwa mshahara wa hadi Sh24 milioni kwa wiki ugani Wembley.

Kwa mujibu wa kocha huyo wa zamani wa Southampton, kumhusisha na Man-united ni sawa na jitihada za kumlazimishia ‘mpango wa kando’ wakati ambapo mkewe halali (Tottenham) anamridhisha vilivyo. Pochettino amekuwa akidhibiti mikoba ya Tottenham tangu 2014 alipoagana na Southampton. Kulingana naye, msimu huu umekuwa mbaya kwake hasa baada ya kucheleweshwa kwa tarehe ya kufunguliwa kwa uwanja mpya wa Tottenham ambao pia hawakujishughulisha vilivyo katika soko la uhamisho muhula huu.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Kenya

© PressReader. All rights reserved.