Gavana Nyong’o asa rishwa Nairobi kwa matibabu maalum

Taifa Leo - - FRONT PAGE - NA MAGDALENE WANJA

WAKAZI wa Kagoto, eneobunge la Bahati, Kaunti ya Nakuru jana walivamia kampuni inayotengeneza kokoto eneo hilo, wakitaka ifungwe baada ya milipuko kutoka kwa machimbo ya mawe kuharibu nyumba zao.

Kulingana na wenyeji hao waliofunga barabara ya Nakuru-nyahururu, mlipuko kutoka eneo la uchimbaji mawe Jumamosi ulisababisha tetemeko la ardhi lililoacha nyumba zao na nyufa.

Bi Rose Wairimu, moja wa waandamananji alidai kwamba kisa hicho si cha kwanza na visa hivyo vimezidi kutokana na uchimbaji wa mawe uliokithiri.

‘Nyumba zetu sasa zimejaa mawe yanayoingia ndani kupitia kwa paa wakati wa uchimbaji wa mawe hayo,” akasema. Wenyeji hao waliitaka serikali kuingilia kati la sivyo maafa makubwa huenda yakatokea siku za usoni kutokana na shughuli hizo za uchimbaji.

Hata hivyo Mkuu wa polisi wa Bahati, Bw Edward Wafula, aliyethibitisha kisa hicho, alitangaza kusitishwa kwa shughuli zote za uchimbaji hadi maelewano kati ya wadau wote yaafikiwe.

“Tumepokea malalamiko kutoka kwa wakazi na tayari tumesimamisha shughuli za uchimbaji ili watu wazungumze,” akasema.

Picha/john Njoroge

MBUNGE wa Bahati Kimani Ngunjiri akihutubia wakazi nje ya kampuni ya ujenzi ya Karsan Ramji and Sons . Wakazi wamelalama kuwa shughuli za kampuni zinaathiri majengo yao.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Kenya

© PressReader. All rights reserved.