Swazuri alaumiwa kwa kupuuza matatizo ya ardhi Pwani

Taifa Leo - - FRONT PAGE - Na CHARLES LWANGA

MBUNGE wa Magarini Michael Kingi ametaja Tume ya Ardhi (NLC) kuwa kizingiti kikuu katika kumaliza dhuluma za kihistoria kuhusiana na mashamba eneo la Pwani.

Bw Kingi alisema tume hiyo, ambayo inaongozwa na Muhammad Swazuri, imekosa kutatua shida za mashamba eneo la Pwani tangu Katiba mpya ilipopitishwa miaka tisa iliyopita.

Mbunge huyo alisema Prof Swazuri ameendelea kuchangia pakubwa katika dhuluma hizo badala ya kutafuta suluhisho kwa tatizo la wenyeji wa Pwani kukosa ardhi na wengi kuishi kama maskwota kwenye mashamba ya mababu zao.

MBUNGE wa Magarini Michael Kingi amedai kuwa Tume ya Ardhi Nchini (NLC) ndiyo kizingiti katika vita dhidi ya dhuluma za kihistoria kuhusiana na mashamba eneo la Pwani.

Bw Kingi alisema tume hiyo ambayo inaongozwa na Prof Muhammad Swazuri imekosa kutatua shida za mashamba eneo la Pwani tangu Katiba mpya ilipopitishwa miaka tisa iliyopita.

Akizungumza alipohudhuria mazishi eneo la Sabaki, mbunge huyo alisema Prof Swazuri amezidi kuchangia pakubwa katika dhuluma hizo badala ya kutimiza ahadi ya kutatua mizozo kama inavyostahili. “Kama kuna adui wa Wapwani kuhusiana na mashamba ni mwenyekiti wa NLC Swazuri, sisi hulalamika kila mara kutokana na dhuluma na badala ya kutusaidia kama mkazi wa Pwani ambaye anaelewa shida hizi, yeye ndiye sasa anagawia mabwenyenye mashamba yetu,” alisema.

Bw Kingi alisema itakuwa shida kupata msomi mwingine kutoka Pwani kuongoza nafasi hiyo baada ya Prof Swazuri kustaafu Februari au Machi.

“Jambo la kushangaza ni kuwa wakati mtu wa Pwani anachaguliwa kuchukuwa nafasi hiyo anageuka kuwa adui ya Wapwani wenzake na mambo haya yakitendeka mnataka sasa sisi viongozi tufanye vipi?” akauliza.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Kenya

© PressReader. All rights reserved.