Mbunge aapa kukosoa serikali ya kaunti

Taifa Leo - - NEWS - NA STEVE NJUGUNA

MBUNGE Mwakilishi wa Wanawake katika Kaunti ya Laikipia, Bi Catherine Waruguru amesisitiza kuwa ataendelea kukosoa uongozi wa eneo hilo kwa kukosa kutekeleza miradi ya maendeleo ya kuwafaa wakazi.

Hii ni kufuatia kisa cha wiki jana ambapo mkutano ulioandaliwa na Bi Waruguru mjini Nanyuki ulitibuka baada ya vijana kumzomea wakidai anaingilia viongozi wengine.

Bi Waruguru alimlaumu Naibu Gavana, John Mwaniki kwa madai ya kuwakodisha vijana kutibua mkutano wake, huku akisisitiza kwamba serikali ya kaunti hiyo haijafanya chochote kutekeleza miradi ya maendeleo katika kaunti hiyo.

“Naibu Gavana aliwakodisha vijana kuharibu mkutano wangu. Vijana hao hata walinifichulia kwamba walipewa fedha ili kuzua vurugu,” akaeleza Bi Waruguru.

“Ukosefu huo wa miradi umechochea ofisi yangu kudhamini baadhi ya miradi inayofaa kutekelezwa na serikali ya kaunti,” akaongeza.

Lakini Bw Mwaniki alipuuzilia mbali madai ya mbunge huyo akisema hana muda wa siasa zisizo za maendeleo.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Kenya

© PressReader. All rights reserved.