LSK yataka Maraga aagize kuundwa kwa mahakama maalum za wikendi

Taifa Leo - - NEWS - Na Sam Kiplagat

CHAMA cha Mawakili wa Kenya (LSK) sasa kinamtaka Jaji Mkuu David Maraga aagizwe kuunda mahakama maalumu za kusikiliza kesi wikendi na sikukuu za kitaifa.

Kwenye kesi iliyowasilishwa kwa dharura, LSK inasema mahakama hizo maalumu zitazuilia washukiwa kufungwa seli zaidi ya saa 24 zinazoruhusiwa kikatiba.

Chama hicho kilieleza wasiwasi kuhusu mtindo wa kukamata washukiwa Ijumaa mchana, ambao umekuwa maarufu kama 'Kamata-kamata'.

Kulingana na mawakili hao, mshukiwa anapokamatwa Ijumaa mchana huwa ni vigumu kwake kufikishwa mahakamani kabla saa 24 zikamilike kwa hivyo wananyimwa dhamana na kukaa kizuizini hadi Jumatatu.

Wanataka pia Jaji Maraga apange ratiba ya majaji na mahakimu kuwa kazini katika kila mahakama nchini kote wikendi, sikukuu za kitaifa na baada ya saa rasmi za kikazi ili kushughulikia masuala yoyote ya dharura yanayohusu ulinzi wa haki za binadamu.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Kenya

© PressReader. All rights reserved.