Mmoja afariki kwenye ajali huku wengine wanane wakijeruhiwa

Taifa Leo - - NEWS - Na George Munene

MTU mmoja alifariki huku wengine wanane wakijeruhiwa vibaya kwenye visa tofauti vya ajali mjini Embu mnamo wikendi.

Ajali ya kwanza ilitokea baada ya lori moja kuanguka karibu na Mto Itabua baada ya dereva kupoteza udhibiti wake.

Dereva huyo alifariki papo hapo huku abiria wawili waliokuwa wameabiri wakapata majeraha ya shingo na miguu.

Walioshuhudia walisema kwamba waliliona lori hilo likiondoka barabarani kabla ya kubingiria mara kadhaa.

“Nadhani dereva alipoteza udhibiti wake baada ya breki zake kukosa kufanya kazi,” akasema mmoja wa walioshuhudia.

Katika soko la Kiritiri, watu sita walijeruhiwa baada ya gari la kusafirishia miraa kuhusika katika ajali.

Gari hilo lilikuwa likisafirisha zao hilo Nairobi kutoka Mbeere, wakati ajali hiyo ilipotokea. Kulingana na walioshuhudia, gari hilo liligonga shimo na kupoteza mwelekeo.

“Dereva alipoteza udhibiti wake, ambapo lilibingiria na kujeruhi abiria wote sita waliokuwa ndani,” akasema Bw Njeru Kamagambo.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Kenya

© PressReader. All rights reserved.