Mbunge ashauri kuhusu siasa 2022

Taifa Leo - - HABARI ZA KAUNTI -

Na LAWRENCE ONGARO

VIONGOZI wamehimizwa kuangazia ajenda nne za serikali badala ya kujadili siasa za mwaka wa 2022.

Mbunge Mwakilishi wa Wanawake katika Kaunti ya Kiambu, Bi Gathoni Wa Muchomba, alisema viongozi wengine wamebuni mbinu ya kujitakia makuu kwa kujadili maswala ya urithi wa rais.

Akizungumza katika shule ya upili ya Gatei alipowasilisha tangi la maji la lita 5,000, Bi Wamuchomba alisema viongozi wenyewe ndio wanastahili kuleta maendeleo katika maeneo yao ya uwakilishi.

"Kila kiongozi ana fedha za CDF ambazo ni za kuleta maendeleo katika maeneo, na kwa hivyo waendelee kufanyia wananchi kazi halafu siasa za 2022 zitafikiriwa baadaye," alisema.

Alimhimiza Rais Uhuru Kenyatta, kuendelea kutekeleza ajenda zake hasa kuunganisha Wakenya na asikubali kutatizwa na viongozi wanaotaka kupata umaarufu kupitia ajenda ya urithi.

Picha/maktaba

MWAKILISHI wa Wanawake Kaunti ya Kiambu, Gathoni Muchomba.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Kenya

© PressReader. All rights reserved.