Wafanyabiashara wazozania pesa walizochangiwa

Taifa Leo - - HABARI ZA KAUNTI -

Na SHABAN MAKOKHA

UHASAMA mkubwa umeibuka kati ya wafanyabiashara wadogo mjini Kakamega kuhusu pesa zilizochangishwa na wanasiasa ili kuwanunulia basi.

Hii ni baada ya makundi mawili ya wafanyabiashara hao kulaumiana kuhusu matumizi mabaya ya zaidi ya Sh3.2 milioni zilizochangishwa wakati wa harambee iliyohudhuriwa na kiongozi wa chama cha ANC Musalia Mudavadi, Mwenyekiti wa chama cha KANU Gideon Moi, maseneta James Orengo na Cleophas Malala wa Siaya na Kakamega mtawalia na baadhi ya wabunge.

Kundi linaloongozwa na mwenyekiti wa Kakamega Traders Sacco, Joseph Oyolo limemshtumu lile la Muungano wa wafanyabiashara wa Kakamega, kwa kutoeleza zilipo fedha zilizokusanywa kutoka kwa wafanyabiashara wadogo wadogo kabla ya mchango huo.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Kenya

© PressReader. All rights reserved.