Polisi wachunguza moto katika shule

Taifa Leo - - HABARI ZA KAUNTI - Na Titus Ominde

Mali ya thamani isiyojulikana iliharibiwa na moto ulioteketeza mabweni manne na madarasa mawili katika shule ya upili ya Ainabkoi katika kaunti ya Uasin Gishu wikendi.

Afisa mkuu wa polisi Eldoret Mashariki, Bw Richard Omanga, alisema moto huo ambao kiini chake hakijajulikana ulianza majira ya saa mbili unusu usiku wa Ijumaa.

Moto huo ulianzia kwenye bweni moja wakati wanafunzi walikuwa kwenye masomo yao ya ziada.

Bw Omanga alisema moto huo uliharibu mali ya wanafunzi ikiwemo nguo, malazi na vitabu miongoni mwa vitu zingine.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Kenya

© PressReader. All rights reserved.