Mbunge ataka wakazi wasisahau elimu kwa kupenda harusi zaidi

Taifa Leo - - KURUNZI YA PWANI - Na Fadhili Fredrick

MBUNGE wa Matuga, Bw Kassim Tandaza amewahimiza wazazi kuzingatia na kuwekeza katika elimu ya watoto wao badala ya kuweka juhudi zaidi katika shughuli za kijamii kama sherehe za harusi.

Bw Tandaza alisema wazazi wengi katika eneobunge lake wanapeana kipaumbele zaidi kwa harusi na matukio mengine ya kijamii kuliko elimu.

Pia alisema wazazi hutumia pesa zao kwa sherehe hizo bila kuangalia maslahi ya elimu.

"Tunapaswa kuipatia kipaumbele na kuwekeza katika elimu ambayo itahakikisha maisha mazuri ya watoto wetu na vizazi vijavyo," akasema.

Alisema wazazi hutumia muda mwingi na pesa katika michango ya harusi badala ya kuzingatia elimu.

Mbunge huyo aliwahimiza wazazi kushirikiana na walimu ili kuboresha matokeo na viwango vya elimu.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Kenya

© PressReader. All rights reserved.