Wataka viongozi wa Likoni washirikiane

Taifa Leo - - KURUNZI YA PWANI - Na Hamisi Ngowa

BARAZA la wazee, katika eneo bunge la Likoni Mombasa limeanzisha mpango wa kuwakutanisha na kupatanisha viongozi wa kisiasa katika eneo hilo.

Katika kikao na wanahabari, viongozi wa baraza hilo walisema wakati umefika kwa wanasiasa wa eneobunge hilo kuiga mfano wa Rais Uhuru Kenyatta na kinara wa muungano wa upinzani, Bw Raila Odinga.

Katibu mratibu wa baraza hilo, Bw Ali Sudi Mwasirima alisema uhasama wa kisiasa ambao umeendelea kushuhudiwa kwa zaidi ya miaka 20 umelemaza juhudi za kuimarisha maendeleo katika eneobunge hilo.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Kenya

© PressReader. All rights reserved.