Ouko mulika hela za SMS Knec

Taifa Leo - - BARUA -

AFISI ya Mhasibu Mkuu Edward Ouko inafanya kazi nzuri kufichua utumizi mbaya wa fedha za umma. Kila mwaka KNEC hutumia nambari ya SMS kuarifu watahiniwa wa Mtihani wa Kitaifa wa Shule za Msingi (KCPE) na wa upili (KCSE) matokeo yao. Mwaka uliopita kulikuwa na watahiniwa karibu milioni 1.6 wa mitihani hiyo.

Kuna matukio ambapo matokeo ya mwanafunzi mmoja huangaliwa na watu zaidi ya mmoja wakiwemo walimu, wazazi, jamaa na marafiki na kila ujumbe hugharimu Sh25. Inafaa tuambiwe hizi pesa hutumiwa vipi. VERONICA ONJORO, Mombasa

Newspapers in Swahili

Newspapers from Kenya

© PressReader. All rights reserved.