Viongozi tulieni mchape kazi, siasa za 2022 zisitukoseshe maendeleo nchini

Taifa Leo - - BARUA -

KWA kweli ni jambo la kukera sana tunaposhuhudia viongozi wanaostahili kuwa kielelezo bora kwa wananchi wanapotupiana cheche za maneno hadharani.

Yote haya yanachangiwa na siasa za mwaka wa 2022 ambao kwa kweli u mbali sana.

Sioni ni kwa nini viongozi hawa warushiane maneno kila kuchao huku kazi ambazo tuliwachagua watufanyie zikiwa bado hazijakamilika.

Viongozi, itakuwa jambo la kistaarabu iwapo mtawajibikia kazi ambazo tuliwachagua mtufanyie.

Siasa ambazo zitasababisha mgawanyiko kwa wananchi tuache.

Uwajibikaji wenu katika kazi tulizowachagua ili mtufanyie ndio utatufanya sisi wananchi tuamue iwapo mnastahili kupewa uongozi tena au la. Kwa hivyo, wajibikeni katika huduma na muache siasa zinazosababisha kurushiana cheche za maneno.

ZEWEDI MANG'ENI COLLINS,

Mombasa

Newspapers in Swahili

Newspapers from Kenya

© PressReader. All rights reserved.