Tuwe na muafaka wa referenda

Taifa Leo - - BARUA -

MJADALA kuhusu marekebisho ya Katiba unafaa kufanywa kwa busara.

Kufikia sasa kumekuwa na watu wengi wanaozungumzia suala hili ilhali hakuna mwelekeo wowote mwafaka.

Kila upande unaonekana kujitokeza na mapendekezo yake huku kukiwa na wengine wanaopinga marekebisho hayo.

Ingekuwa bora iwapo makundi haya mawili yangejadiliana ili kuwe na mwongozo mmoja.

Baada ya hapo, tupate kujua nini kinatakikana kurekebishwa ndipo wanaopinga pia watuambie wanachopinga.

Kwa sasa kuna wanaokusanya saini ilhali kuna uwezekano hilo litavurugwa na ukusanyaji saini mwingine baadaye.

PETER KIMANI, Nairobi

Newspapers in Swahili

Newspapers from Kenya

© PressReader. All rights reserved.