Barca kumuuza Coutinho ndipo warejeshe Neymar

Taifa Leo - - GUMZO LA SPOTI -

PHILIPPE Coutinho anapitia wakati mgumu kupata namba Barcelona mwaka mmoja tu baada ya kutua uwanjani Camp Nou kwa Sh16.3 bilioni kutoka Liverpool. Habari zinasema huenda Mbrazil huyu akauzwa mwisho wa msimu huu ili kuchangisha fedha za kuajiri tena Neymar. Coutinho alijiunga na Barca mwezi Januari mwaka 2018 na hakuweza kushiriki Klabu Bingwa Ulaya, lakini aliridhisha katika nusu ya pili ya msimu akipachika mabao 10 katika mechi 22 Barca ikishinda Ligi Kuu na soka ya Copa del Rey. Hata hivyo, amepata maisha yamekuwa magumu katika msimu wake wa pili akianzishwa mechi moja pekee kati ya tano zilizopita iliyotama-

Newspapers in Swahili

Newspapers from Kenya

© PressReader. All rights reserved.