AS Monaco, Everton vitani kumsajili nyota Batshuayi

Taifa Leo - - GUMZO LA SPOTI -

GUMZO limeibuka kwamba Monaco sasa inaongoza katika vita vya kupata huduma za mshambuliaji wa Chelsea, Michy Batshuayi baada ya kipindi cha mkopo katika klabu ya Valencia kukatizwa. Tovuti ya Goal inasema kwamba wakala wake Meissa N’diaye amewasili Monaco kufanya mazungumzo ya kina kuhusu mteja wake kujiunga na klabu hii kutoka Ligi Kuu ya Ufaransa. Everton imekuwa ikiwazia kuomba huduma zake kwa Sh2.3 bilioni kwa sababu haiwezi kumsaini kwa mkopo. Ripoti pia zinasema kwamba Crystal Palace pia inamezea mate Mbelgiji huyu mwenye umri wa miaka 23.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Kenya

© PressReader. All rights reserved.