Mhispania naye ataka kuwa rais wa Amerika

Taifa Leo - - HABARI ZA AFRIKA NA DUNIA - Na AFP

ALIYEKUWA Meya wa San Antonio, Texas na waziri katika serikali ya aliyekuwa Rais Barack Obama amepanga kuzindua azma yake kuwa rais wa kwanza mwenye asili ya Uhispania nchini Amerika.

Julian Castro anachukua hatua hiyo wakati ambapo mjadala umezidi kutokota kuhusu suala la wahamiaji wanaoingia Amerika kutoka mataifa yaliyo nyuma kiuchumi, hasa kutoka Amerika Kusini.

Castro, 44, anatarajiwa kupigania tikiti ya kuwania urais kupitia Chama cha Democratic mwaka wa 2020 dhidi ya vigogo wa kisiasa nchini humo kama vile aliyekuwa makamu wa rais Joe Biden, maseneta Elizabeth Warren, Bernie Sanders na Kamala Harris, na pengine mfanyabiashara bilionea wa madola Michael Bloomberg.

Anategemea zaidi ujuzi wake wa kujieleza mbele ya hadhira, mafanikio aliyoletea taifa alipokuwa Waziri wa Nyumba na alipokuwa meya wa jiji lililo la saba kwa ukubwa Amerika na pia ucheshi wake unaovutia wengi.

Picha/afp

Bw Juliàn Castro akitangaza azma yake kuwania urais Amerika.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Kenya

© PressReader. All rights reserved.