Nyuki kutoka kaburini wamuua mkongwe wakati wa maombi

Taifa Leo - - HABARI ZA AFRIKA NA DUNIA -

Na SAM CALEB OPIO

NYUKI walivamia mkutano wa maombi ya familia katika kijiji cha Kirangira, Kaunti Ndogo ya Nkondo, Wilaya ya Buyende na kumuua mzee mwenye umri wa miaka 80 katika hali isiyoeleweka.

Mzee wa kijamii Zadoko Mulamba, alivamiwa na nyuki hao waliodaiwa kutoka kwa kaburi la mjukuu wake, Kirabo Taligoola, ambaye alifariki kwenye ajali barabarani mwaka uliopita.

Ilidaiwa mjukuu huyo amekuwa akilalamika kaburini kwamba 'wageni' wanatatiza usingizi wake ndiposa familia ikaitisha mkutano wa maombi.

Watu wengine watatu wa familia hiyo walijeruhiwa vibaya wakakimbizwa hadi katika zahanati ya Nkondo.

Askofu Eddie Munene wa Kanisa la Born Again Churches lililo Busoga, alisema watu walio na imani katika nguvu za mapepo hawana uwezo wa kukabiliana na nguvu hizo.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Kenya

© PressReader. All rights reserved.