Malengo yake makuu Jemima ni kutandaza soka ya ligi Uingereza

Taifa Leo - - DIMBA - NA ABDULRAHMAN SHERIFF Dimba Alone’ ‘You’ll Never Walk Picha/abdulrahman Sheri

KILA mchezaji hupania kujishirikisha katika mchezo anaoupenda kwa ajili ya kuendeleza talanta yake akiwa na nia ya kufikia kilele cha kumfanya atambulike kuwa maarufu katika mchezo huo.

Jemima Charo ambaye ni mwanafunzi wa Kidato cha Nne katika Shule ya Upili ya Ngala Memorial iliyoko Matsangoni aliamua kujiunga na uchezaji wa soka alipokuwa shule ya msingi akiwa kwa nia ya kuwa mmoja wa wachezaji bora katika kijiji cha Kitsoeni, Wadi ya Chasimba, Kaunti ya

Kilifi.

Kwamba Jemima anacheza kandanda si kwa ajili ya kujiweka katika hali ya afya pekee ama kushindania nafasi katika kikosi cha kwanza cha timu yake ya Kitsoeni Princess FC bali azma yake kubwa ni kuhakikisha anapata fursa ya kuichezea timu ya soka ya wanawake ya Liverpool

FC.

“Nikiwa shabiki sugu wa Liverpool FC ya

Uingereza, ninajitahidi kufikia kiwango cha kuichezea timu ya soka ya wanawake ya klabu hiyo ya Liverpool. Nimeweka nia na ninaamini utafika wakati nitaweza kukipiga katika kikosi cha timu hiyo,” anasema chipukizi huyo.

Aliambia

kuwa atajitahidi kuendeleza kipaji cha uchezaji wake akitia nia ya kuichezea mojawapo ya klabu kubwa hapa nchini inayoshiriki kwenye Ligi

Kuu ya Soka ya Wanawake kwani anaamini ni katika ligi hiyo ndipo atatambulika na kuonekana na maskauti. “Ninaipenda sana timu ya Liverpool na hasa moto wake ule wa unanivutia sana na sitamaliza hamu yangu ya kuwa mchezaji mzuri hadi pale nitakapovaa jezi ya timu hiyo na kuteremka uwanjani kwa mechi za Ligi Kuu ya soka ya kina mama huko Uingereza,” akasema Jemima.

Mwanasoka huyo ambaye ndiye mfungaji bora wa timu yake ya hiyo ya Kitsoeni Princess FC anasema anatamani sana wakufunzi wa timu ya taifa ya Harambee Starlets awe akitembelea mashinani kushuhudia wanasoka wenye vipaji.

“Nina imani kubwa maafisa wa soka wa benchi ya ufundi wa timu ya taifa ya Starlets wakija sehemu za mashinani, watapata wachezaji wazuri wenye talanta na ambao wataweza kuteuliwa kwenye kikosi cha timu hiyo,” akasema Jemima.

Alitoa ombi pia kwa maskauti kutoka ng’ambo wawe wakikaribishwa kushuhudia mechi za michezo ya shule za msingi na upili kwani ni kutokana na michezo hiyo, ndipo hutokeza chipukizi wenye vipaji vya hali ya juu vya kusakata soka. Kocha wake Alex Mwakadi anasema Jemima ni mchezaji mwenye ari ya kujiendeleza kisoka na anaamini anaweza kuwa mwanasoka mwenye kutajika miaka michache ijayo. “Jemima ni mmoja wa wanasoka wa kike wenye nia ya kupiga hatua hadi kucheza Ligi Kuu ya Uingereza,” akasema.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Kenya

© PressReader. All rights reserved.