Legend FC yaanza ligi kwa kulaza Lakeview

Taifa Leo - - SPOTI - Na Titus Maero

LEGEND FC ilianza kampeni ya kusaka ubingwa wa Ligi ya Kitaifa ya Daraja ya pili ya Kanda ya Magharibi ya Zoni A kwa kupepeta Lakeview FC 1-0 katika Shule ya Upili ya Roasterman, Jumamosi. Bao la pekee na la ushindi la Legend ya mkufunzi Hezron Okumu, lilifumwa wavuni na mvamizi matata Eliud Otieno dakika ya 67. Katika mchuano mwingine, Busia Olympic FC ililima timu ya Chuo Kikuu cha Masinde Muliro almaarufu MMUST FC 1-0 mjini Busia.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Kenya

© PressReader. All rights reserved.