Fabregas sasa mali rasmi ya Monaco ya mkufunzi Henry

Taifa Leo - - SPOTI -

mipira 10 pekee ndani ya nyavu zao baada ya michuano 22 ligini.

Ushindi wa Liverpool uliendeleza ubabe wao katika kampeni za EPL msimu huu. Kwa sasa, wanaselelea kileleni mwa jedwali kwa alama 57 huku wakijivunia pengo la alama 16 kati yao na Arsenal.

Chini ya kocha Unai Emery, Arsenal waliduwazwa kwa kichapo cha 1-0 kutoka kwa West Ham United katika mchuano uliochezewa ugani London mnamo Jumamosi.

Liverpool kwa sasa wanajiandaa kuwaalika Crystal Palace uwanjani Anfield mwishoni mwa wiki hii huku Brighton wakiwaendea Manchester United ugani Old Trafford.

Kwa mujibu wa Klopp, ushindi wao dhidi ya Brighton ugenini unatarajiwa kuwa kiini cha hamasa yao wanapojiandaa kwa sasa kukabiliana na ratiba ngumu iliyopo mbele yao.

“Nawapongeza wachezaji wangu kwa ushindi huu muhimu. Sisemi lolote kuwahusu wapinzani wetu wakuu. Kila timu ingali vitani. Kosa kubwa litakalofanywa na Liverpool kwa sasani kuanza

kuwabeza wapinzani au kulegeza kamba. Hatuwezi kabisa kupuuza kikosi chochote kilichopo ndani ya mduara wa sita-bora kwa sasa,” akaongeza Klopp.

Kulingana na kocha huyo mzawa wa Ujerumani, ukubwa wa viwango vya ushindani katika kampeni za EPL msimu huu huenda ukafanya mshindi wa EPL kuamuliwa katika majuma ya mwisho. Awali, kocha Pep Guardiola wa Man-city alisema Liverpool wanajivunia kikosi imara kilicho na uwezo wa kutwaa ubingwa msimu huu.

Ukiwa na suala lolote ungetaka kuwasilisha kwetu, tuma sms bila malipo kwa

KIUNGO Cesc Fabregas amejiunga rasmi na kikosi cha AS Monaco kinachoshiriki Ligi Kuu ya Ufaransa (Ligue 1) chini ya kocha Thierry Henry kwa mkataba wa miaka mitatu na nusu.

Katika mchuano wake wa mwisho ndani ya jezi ya Chelsea, Fabregas ambaye pia amewahi kuwachezea Arsenal na Barcelona, alipokezwa utepe wa unahodha dhidi ya Nottingham Forest katika Kombe la FA. Fabregas alijiunga na Chelsea kutoka Barcelona mnamo 2014 baada ya kuwasakatia Arsenal jumla ya mechi 303 kati ya 2003 na 2011.

Katika kipindi cha usogora wake kambini mwa Chelsea, Fabregas alikishindia kikosi hicho mataji mawili ya EPL, mawili ya Komba la FA na ubingwa wa League Cup baada ya kupiga jumla ya mechi 501. Akivalia jezi za Arsenal, aliwashindia waajiri wake hao wa zamani Kombe la FA na kuwachochea kushiriki fainali ya UEFA mnamo 2006 dhidi ya Barcelona waliomsajili miaka mitano baadaye.

ukianza na neno ‘Taifa’

Newspapers in Swahili

Newspapers from Kenya

© PressReader. All rights reserved.