Azuia mume aliyekesha nje kuwasalimu watoto wake

Taifa Leo - - DONDOO! - Na STEPHEN DIK

Mama mmoja mtaani humu alimkataza mumewe aliyekesha nje kwa siku mbili kusalimia watoto. Yasemekana jamaa alirudi nyumbani baada ya siku mbili na mkewe akamkataza kusalimia watoto akidai alitoka kufanya uasherati.

Mama alisema kulingana na mila na desturi za jamii, baba hastahili kusalimia mtu yeyote nyumbani akitoka kula ufuska. Juhudi za jamaa kumwambia mkewe kwamba alikuwa safarini kikazi hazikufaulu hata kidogo.

Hata hivyo mambo yalitulia pale jamaa alipandwa na hasira na kutisha kurudi alikotoka.

Jamaa alisema alitoka kazini na kama mkewe hakuamini angerudi na kusahau boma hilo kabisa.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Kenya

© PressReader. All rights reserved.