PLUIJM AMVUTA NGOMA AZAM

Bingwa - - MBELE - NA WINFRIDA MTOI

STRAIKA wa Yanga SC, Donald Ngoma, huenda msimu ujao akaonekana katika jezi ya Azam FC, kutokana na kuwa kwenye orodha ya wachezaji watakaotua na kocha anayetarajiwa kukinoa kikosi hicho, Hans van der Pluijm.

Ngoma, anayesumbuliwa na majeraha kwa sasa na ameshindwa kufanya vizuri msimu huu wa Ligi Kuu Tanzania Bara, lakini pia kuna taarifa uongozi wa timu yake uko mbioni kuvunja mkataba wake.

Inadaiwa kuwa, Pluijm baada ya kuhakikishiwa kibarua Azam FC, tayari ameshaanza kupanga kikosi kazi chake, huku akilenga zaidi wachezaji aliofanya nao kazi kwa mafanikio na jina la Ngoma limechukua nafasi kubwa.

Taarifa ilizozipata BINGWA kutoka kwa mtu wa karibu na kocha huyo, zinasema baada ya Pluijm kushindwa kumsajili Ngoma katika kikosi cha Singida kutokana na kubanwa na mkataba wake, anafanya jitihada za kuhakikisha kipindi hiki anamnasa.

Chanzo hicho kilisema kuwa, Ngoma na Pluijm ni watu wanaowasiliana mara kwa mara na hata kipindi hiki ambacho mchezaji huyo ni majeruhi huwa anaulizia maendeleo yake.

“Kama Yanga watakubali kumuachia Ngoma moja kwa moja anakwenda na Hans, kwa sababu anaikubali sana kazi yake na kipindi cha nyuma isingekuwa Yanga kumwongezea mkataba, angekuwa naye Singida United,” kilisema chanzo hicho.

Tofauti na Ngoma, wachezaji wengine ni Adam Salamba wa Lipuli FC na Tafadzwa Kutinyu wa Singida United, ambao tayari uongozi wa Azam umetuma barua.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.